MALI-UFARANSA-AFRIKA-UCHUMI

Emmanuel Macron kuzuru Morocco tarehe 14 na 15 Juni

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuzura baadhi ya nchi barani Afrika.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuzura baadhi ya nchi barani Afrika. REUTERS/Charles Platiau

Morocco ni nchi ya kwanza ya Kiarabu barani Afrika ambayo rais wa Ufaransa anatazamia kuzuru tangu kuchaguliwa kwake mwezi Mei mwaka huu. Rais emmanuel Macron pia atazuru Algeria, katika wiki zijazo, kulingana na taarifa ya Ofisi ya rais iliyowasilishwa katika ofisi ya shirika la habri la Reuters.

Matangazo ya kibiashara

"Rais Emmanuel Macron atafanya ziara ya kiserikali nchini Morocco tarehe 14 na 15 Juni," chanzo katika Ikulu ya Elysee kiliowasiliana na gazeti la Jeune Afrique kimeeleza. Kwa mujibu wa chanzo hiki rais wa Ufaransa atakutana na Mfalme Mohammed VI wakati wa ziara yake. "Hii ni ziara ya hadhi ya kisiasa. Nchi hizi mbili zitajadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wao, "alisema kwa upande wake, afisa wa ngazi ya juu wa Morocco.

Ziara hii, ambayo awali ilielezwa na mtandao wa Atlasinfo siku ya Jumatano Juni 7, ni ya kwanza kwa Emmanuel Macron nchini Morocco baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Ufaransa. Alizuru Tunisia mwezi Novemba, kabla ya kutangaza kugombea kwake katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, na alizuru Algeria mwezi Februari, wakati wa kampeni za urais.

Katika mahojiano na gazeti la Jeune Afrique kabla ya kuchaguliwa kwake, Emmanuel Macron aliahidi kufanya ziara yake ya kwanza nchini Morocco. "Tayari nilizuru Algeria na Tunisia, sijaweza kuzuru Morocco, lakini nitazuru nchi hiyo haraka sana baada ya kuchaguliwa kwangu, kama wananchi wa Ufaransa wataniamini na kunichagua," alisem aEmmanuel Macron.

Ufaransa ni moja ya wawekezaji wa kwanza wa kigeni nchini Morocco. Siku ya Alhamisi, Juni 15, shughuli za awamu ya kwanza za kukarabati kiwanda cha PSA Kenitra zitazinduliwa na rais wa PSA, Carlos Tavares, na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Morocco, Moulay Hafid Elalamy. Hii ni moja ya uwekezaji mkubwa wa Ufaransa nchini Morocco, pamoja na ile ya Renault Nissan.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, rais wa Ufaransa atazuru"katika wiki zijazo" Algeria. Ziara hii iliamuliwa wakati wa mazungumzo ya simu kati ya Emmanuel Macron na Abdelaziz Bouteflika ambapo viongozi hawa wawili walijadili kuhusu hali inayoendelea nchini Libya

Paris inajaribu kuendesha sera ya uwiano kati ya nchi hizi mbili Kiarabu ambazo ni majirani, na zimeendelea kuzozana kuhusu suala la Sahara ya Magharibi. Mvutano kati ya Morocco na Algeria umeeongezeka tangu kurudi kwa Morocco katika Umoja wa Afrika (AU) mwezi Januari mwaka huu.