AFRIKA KUSINI

GuptaLeaks Afrika Kusini: Malema asema barua pepe zilizovuja ni za kweli

Julius Malema, kiongozi wa chama cha  EFF, (Kulia) akiwa na wabunge wengine
Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF, (Kulia) akiwa na wabunge wengine REUTERS/Siphiwe Sibek

Kiongozi wa chama cha EFF nchini Afrika Kusini, Julius Malema, amesema kuwa barua pepe zilizovuja kwa vyombo vya habari kwa wiki mbili ni sahihi na kwamba rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na baadhi ya mawaziri wake wanapora mali ya umma.

Matangazo ya kibiashara

Barua pepe hizo zilizofichuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini zinaonyesha ushirikiano kati ya wajumbe wa baraza la mawaziri, familia ya rais wa Afrika Kusini na familia ya wafanyabiashara tajiri ya Gupta.

Julius Malema amesema, “Barua pepe hizi ni sahihi na zinathibitisha yale chama chake kimekuwa kikishutumu kwa miezi kadhaa sasa.”

Hali hii inamaanisha kuwa rais Jacob Zuma na baadhi ya Mawaziri wake wamedhibitiwa na familia ya Gupta.

Na kwa msaada wao wamekua wakipora mali ya nchi. Ushahidi ni, kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha EFF, rais Jacob Zuma wala mawaaziri wake hawakufungua mashitaka dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vilichapisha barua pepe hizo zinazowaweka hatarini.

Kiongozi wa chama cha EFF anadai kuwa rais Jacob Zumai ana nyumba katika mji wa Dubai - kama zinavyoeleza barua pepe hizi - na Mamilioni ya Euro, yalioporwa kutoka makampuni ya serikali, yaliwekwa kwenye benki nje ya nchi.

Malema ameshutumu hasa Waziri mpya wa Fedha , mshirika wa karibu wa rais wa afrika Kusini, kwa kuhusika na uporaji huo huku akitishia kutoa malalamiko yake mbele ya vyombo vya sheria.