Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Umoja wa mataifa wataka uchunguzi wa kimataifa ufanyike Kasai ya kati nchini DRC, waingereza washiriki uchaguzi wa wabunge

Sauti 20:20
Bwana Zeid Ra'ad al Hussein, mkuu wa tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu, mjini Kinshasa, kwenye mkutano na wanahabari Julai 21 2016
Bwana Zeid Ra'ad al Hussein, mkuu wa tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu, mjini Kinshasa, kwenye mkutano na wanahabari Julai 21 2016 ©RFI/Hadibou Bangré

Makala hii imeangazia ombi la mkuu wa tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu kutaka kufanyike uchunguzi wa kimataifa kuhusu mauaji na uhalifu unaoshuhudiwa kwenye jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, mawaziri wa fedha kwenye nchi za ukanda wa afrika mashariki kuzisoma badgeti za nchi zao kwa pamoja, nchi ya Rwanda kuwarejesha raia 91 wa Burundi, lakini pia kimataifa tumegusia hali ya mvutano kati ya raia wa Marekani Donald Trump na aliyekuwa mkuu wa zamani wa shirika la upelelezi la FBI, James Comey.Ungana nami Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi.