DRC-MACHAFUKO-USALAMA

Kifo cha Kamuina Nsapu, kiongozi wa kimila

Nyumba ya mkuu Kamuina Nsapu katika kijiji kiliopewa jina lake. iliyoteketekezwa baada ya mashambulizi ya jeshi yaliosababisha kifo chake mnamo mwezi Agosti.
Nyumba ya mkuu Kamuina Nsapu katika kijiji kiliopewa jina lake. iliyoteketekezwa baada ya mashambulizi ya jeshi yaliosababisha kifo chake mnamo mwezi Agosti. RFI/Sonia Rolley

Hii ni hadithi ya cheche iliogeuka moto. Tarehe 12 Agosti 2016, Prince Jean Mpandi, kwa jina la "Kamuina Nsapu" wa 6, kiongozi wa kabila la Bajila Kasanga, aliuawa katika shambulio dhidi ya nyumba yake katika mkoa wa Kasai ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa mkoa huo walimuona raiai mwengine kutoka mkoa wa Kasai ya Kati, Étienne Tshisekedi, kiongozi wa kihistoria wa upinzani aliporidi nchini baada ya miaka miwili ya akiwa uhamishoni. Miezi michache kabla ya kumalizika kwa muhula wa Joseph Kabila, mmoja kati ya hao aliweka mbele uasi, mwengine aliyapa kipaumbele mazungumzo. Miezi kumi baadaye, kulishuhudiwa vifo vya mamia ya watu, labda maelfu ya watu, lakini pia maelfu ya watoto kusajiliwa katika kundi la waasi, zaidi ya milioni moja ya watu kuyahama makaazi yao na makaburi yasiopungua arobaini na mbili.

Kama Étienne Tshisekedi, Jean-Prince ni kutoka mkoa wa Kasai ya Kati, moja ya mikoa maskini zaidi ya ukanda wa Grand Kasai. Hadi wakati huo, machafuko bado yanaendelea. Parokia zimejengwa kila kilomita ishirini na vijiji vyenye majina ya wakuu wanaoongoza pembezoni mwa parokia hizo. Barabara ni chache mno na madaraja yaliojengwa na wamisionari na tangu kuondoka kwao hakuna maendeleo yoyote. Hata hivyo barabara ya reli iliyojengwa kando ya mito, bado inafanya kazi.

Etienne Tshisekedi aliukimbia mkoa huu wa Kasai ya Kati kwa muda mrefu na alikua akiendesha vita vyake vya kisiasa katika mji wa Kinshasa. Lakini katika ukanda wa Grand Kasai, kuna taasisi tu tatu zinazojulikana: Serikali, ambayo inapingwa na wengi, Kanisa Katoliki, ambalo limepoteza nafasi, na wakuu wa kimila. Tangu mwaka 2015, sheria mpya inayohusu mamlaka ya viongozi wa jadi ilianza kutekelezwa. Serikali ya Joseph Kabila inatuhumiwa kutumia sheria hiyo mpya kwa malengo ya kisiasa ili kuweka udhibiti wake katika ukanda huo ambao ni makao makuu ya upinzani. Tangu enzi za ukoloni, hakuna utawala- ikiwa ni pamoja na ule wa Mobutu, wala ule wa Laurent Kabila uliothubutu kuingilia kazi za utawala wa kimila katika ukanda wa Grand Kasai. Inasemekana kwamba rais Mobutu mwenyewe alikuwa akiheshimu wakuu muhimu wa kimila, na kuwakuta nyumbani kwao, na kusalimiana nao.

Lakini tangu wakati huo, migogoro kadhaa ya kiuchumi ilishuhudiwa. Mgogoro wa mwisho ni huu unaoikumba wakati huu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tukio ambalo linakumbusha raia wengi wa DR Congo, lile la miaka ya 90 na mwisho wa utawala wa Mobutu: kuanguka kwa fedha za kitaifa, uhaba wa sarafu za kigeni, kupanda kwa bei za bidhaa mahitajio na ukosefu wa ajira. Uchumi wa ukanda wa Grand Kasai unakumbwa na giza kama kampuni ya madini ya Bakwanga (MIBA), ambayo wakati huo ilikua kampuni bora zaidi nchini humo, ambapo kwa wakati huu iko njia pandakatika eneo la Mbuji Mayi na kwa leo inakabiliwa na migo wa madeni yanayokadiriwa kufikia dola milioni 200.

Mwishoni mwa mwaka 2012 Jean-Prince Mpandi alikabidhiwa madaraka na kuwa "Kamuina Nsapu" wa 6, ni kusema moja ya wakuu wa kimila wa eneo la Dibaya katika mkoa wa sasa wa Kasai ya Kati. wakati huo alikua na umri wa miaka 46. mtangulizi wake, Anaclet Kabeya Mupala, alikuwa afisa wa jeshi wakati wa utawala wa Mobutu katika jeshi la Zaire wakati huo (FAZ), jeshi la serikali ya zamani. Alifariki miezi michache baadae katika mazingira ambayo washirika wake wa karibu hawakuamini. Evariste Boshab pia kutoka mkoa wa Kasai ya Kati, wakati huo alikua Spika wa Bunge.

Kamuina Nsapu Ntumba, ambaye nilimrithi, alifariki katika mazingira ya maandalizi ya mkutano na Boshab. Naapa kulinagana na mila yetu, siwezi hata kuongea kwenye simu na Boshab, kwa kuwa anahusika na kifo cha Kamuina Nsapu Ntumba, " Jean Prince Mpandi aliambia kwenye simu ujumbe wa wabunge, Agosti 11, 2016.

Mnamo mwezi Desemba 2014, Evariste Boshab aliteuliwa na Joseph Kabila kuwa naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani na mpinzani mkuu wa Kamuina Nsapu. Evariste Boshab anashtumiwa na wapinzani wake haokuongeza sheria zinazotoa hadhi ya kiongozi wa kimila kwa wasaidizi wake wa kisiasa, na hivyo kuunda maeneo mengine mapya yaliosimamiwa na wakuu wa kimila katika mkoa wa kasai ya Magharibi. alimteua ndugu yake kama mkuu wa chama cha wakuu wa kimila wa Kasai ya Magharibi, akichukua nafasi ya kiongozi alietimuliwa, Seneta Emery Kalamba Wafwana mfalme wa kabila la Bashilange, ambaye alidai kuwa yeye bado halali.

Katika makala haya utafuata sehemu ya pili (2): "Majibu ya askari wa jeshi la DRC: ushahidi kwa picha" na sehemu ya tatu (3): "Msimamo wa Umoja wa Mataifa kwa mgogoro DRC" kwa njia ya uchapishaji wa mfululizo wa mawasiliano na ripoti kutoka shirika la kimataifa.