UFARANSA-BURKINA FASO

Mwanajeshi wa Ufaransa ahukumiwa mwaka 1 jela kwa udhalilishaji wa mtoto wa miaka 3

Mwanajeshi wa Ufaransa akionekana kwenye doria ukanda wa Sahel, hii ni nembo inayotumiwa na jeshi hilo.
Mwanajeshi wa Ufaransa akionekana kwenye doria ukanda wa Sahel, hii ni nembo inayotumiwa na jeshi hilo. REUTERS/Christophe Petit Tesson/Pool

Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela na mahakama ya jijini Paris baada ya kupatikana na hatia ya kumdhalilisha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na mitano kwenye hoteli moja nchini Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi huyo aliyefahamika kwa jina la Sebastien akiwa na mwenzake walirekodi udhalilishaji huo baada ya kuwa marafiki na mmoja wa wazazi wa watoto hao raia wa Ufaransa ambaye aliwaalika kwenye makazi yake.

Hata hivyo waliacha picha za video hiyo nyumbani kwa mama wa watoto hao ambaye aliamua kuipelekea kwenye ubalozi wa Ufaransa ambao nao uliagiza mara moja kurejeshwa nyumbani kwa wanajeshi hao.

Kwa mujibu wa jarida la FranceInfo limeripoti kuwa mwanajeshi huyo alikiri kumdhalilisha kingoni mtoto huyo mjini Ouagadougou na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kikifuatiwa na kifungo kingine cha mwaka mmoja nje.

Mahakama ya Paris pia ilimzuia mwanajeshi hiyo kujihusisha na kazi yoyote kwa muda wa miaka mitano itakayohusisha watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano na kumuagiza kulipa kiasi kdhaa cha Euro kwa familia ya mtoto aliyemdhalilisha.

Mwanajeshi huyu alikuwa nchini Burkina Faso kama sehemu ya kikosi cha Ufaransa kinachopambana na ugaidi kwenye eneo la Sahel.