DRC-MACHAFUKO-USALAMA

Majibu ya jeshi la DRC kufuatia mauaji katika mkoa wa Kasai ya Kati

Machafuko katika mkoa wa Kasi ya Kati, DRC, yamesababidsha vifo vya watu wengi na maelfu kadhaa kulazimika kuyahama makazi yao.
Machafuko katika mkoa wa Kasi ya Kati, DRC, yamesababidsha vifo vya watu wengi na maelfu kadhaa kulazimika kuyahama makazi yao. RFI/Sonia Rolley

Katika miezi kumi, ukanda wa Grand Kasai uliokuwa kwenye amani kwa zaidi ya miaka 40, sasa umegeuka eneo la machafuko. Tangu kifo cha kiongozi wa kijadi Kamuina Nsapu, mamia ya watu, labda maelfu ya watu waliuawa, huku kukigunduliwa angalau makaburi ya halaiki arobaini na mbili na zaidi yawatu milioni moja kuyahama makazi yao.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na uasi uliozuka katika ukanda huo, vikosi vya usalama viliendesha mashambulizi mabaya katika hali ya kuzima kundi hilo la uasi. Walihusika na mauaji hayo wanajulikana.

Vurugu zilizoukumba ukanda wa Grand Kasai zimesababisha wakazi wengi wa ukanda huo kuwapoteza ndugu, jamaa na marafiki. Katika miezi kumi, mgogoro kati ya wafuasi wa mkuu wa jadi Kamuina Nsapu na vikosi vya usalama ulisambaa katika mikoa mitano. Makaburi yasiopungua arobaini na mbili yaligunduliwa, huku watu zaidi ya milioni moja wakilazimika kuyahama makazi yao kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za mashirika ya kibinadamu na mashirika yasio ya kiserikali. Tangu Januari 2017, uasi huo uliozuka uliendelea kushika kasi na kuzuka kwa mgogoro wa kikabila uliochochewa kisiasa. Wakati huo Wafuasi wa Kamuina Nasabu walijibu mashambulizi ya vikosi vya usalama wakidai kuwa wanajihami kama walivyofanya wapiganaji wa Mai-Mai katika vita vya kwanza nchini DRC. Kwa upande wa wanamgambo wa kiongozi huyo wa kijadi walibaini kwamba askari hao, hasa wale ambao walikua katika kundi la waasi lililosaidiwa na Rwanda, ni wavamizi sawa na jeshi la Rwanda.

Mwaka 1996 na 1997,Mia kwa maelfu ya wakimbizi wa Kihutu kutoka Rwanda na raia wa Dr Congo waliouawa kwenye barabara waliokua wakitumia waasi wa kundi la waasi wakati huo la AFDL lililokua likiongozwa na Laurent-Desire Kabila. Kwa wengi, tukio hili lilisahaulika na hakuna hukumu iliotolewa kufuatia mauaji hayo. yote hayo ni mwendelezo wa utamaduni wa ukatili nchini DR Congo. Mauaji yaliyoshuhudia mashariki mwa DRC sawa na yale ambayo yameshuhudiwa hivi karibuni katika ukanda wa Granda Kasai ni sawa na yale yaliotokea nchini Rwanda na Burundi, licha ya kuwa katika nchi hizi mbili mapanga ndio yalitumiwa zaidi kwa mauaji.

Maafisa waliotumwa katika ukanda wa Grand Kasai walianza walianza kazi yao wakati wa mauaji hayo katika nchi hizo. Maafisa au "Kadogo" ni sehemu kubwa ya askari waliotokea mashariki mwa DR Congo ambao walitumwa katika eneo "takatifu" la kiongozi wa jadi Kamuina Nsapu, kwa makubaliano ya jeshi la DRC.

Siku moja kabla ya kifo chake, kiongozi wa jadi Kamuina Nsapu hakufikiria kwamba eneo lake liko katika hatari ya kuanguka katika vurugu hizo. Mbunge mmoja alimuonya: "Kama watu hawa wamekuja kuvamia eneo lako kwa kuua wanawake na watoto, basi fahami kwamba kamwe eneo hili halitokua na amani tena". Lakini Jean-Prince Mpandi hakutaka kusikia hivyo. Hakukubali kusalimu amri kwa serikali na vikosi vyake vya usalama.

Jenerali Eric Ruhorimbere, mpiganaji wa zamani miongoni mwa waliohusika na mauaji

Tarehe 29 Mei 2017,Umoja wa Ulaya uliwawekea vikwazo vipya dhidi ya maafisa tisa wa serikali ya DR Congo. Katika kesi ya ukandamizaji uliotokea katika mkoa wa Kasai ya Kati, Jenerali Eric Ruhorimbere ndie peke alietajwa. Anatuhumiwa kutumia nguvu kupita kiasi na kuwajibika kwa ukandamizaji na mauaji yaliyotekelezwa naaskari katika ukanda wa Grand Kasai.