SOMALIA-USALAMA

Mgahawa wa Posh Treats washambuliwa somalia

Migahawa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, imeendelea kulengwa na mashambulizi mablimbali.
Migahawa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, imeendelea kulengwa na mashambulizi mablimbali. REUTERS/Feisal Omar

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alitekeleza shambulio la mabomu yaliokua yamejazwa katika gari dhidi ya mgahawa maarufu katika mji wa Mogadishu, polisi ya Somalia na mashahidi wamebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alilipua mabomu yaliokua yalijazwa katika gari katika jengo moja mjini Mogadishu, " alisema Ali Mohamed, polisi mjini Mogadishu alisema, na kuongeza kuwa ni mgahawa wa "Posh Treats" ulioshambuliwa. Hakuna idadi ya vifo ambayo imetangazwa, lakini shahidi mmoja, Abas Ahmed, alisema aliona "miili ya watu kadhaa" waliouawa katika shambulio hilo.

Somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi yanayoendeshwa na makundi mbalimbali nchini humo, hasa kundi la Al Shabab.

Hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, licha ya kundi la Al Shabab kunyooshewa kidole na baadhi ya maafisa wa usalama nchini Somalia.

Mashambulizi ya makundi mbalimbali nchini Somalia yamesababisha vifo vya watu wengi na maelfu wengine kuyahama makazi yao na wengine kukimbilia nje ya nchi.