SOMALIA-UGAIDI

Watu 19 wauawa mjini Mogadishu baada ya kushambuliwa na Al Shabab

Shambulizi la bomu katika hoteli maarufu mjini Mogadishu nchini Somalia
Shambulizi la bomu katika hoteli maarufu mjini Mogadishu nchini Somalia sinclairstoryline.com

Watu 19 wameuawa baada ya kundi la kigaidi la Al Shabab kutekeleza shambulizi la bomu mjini Mogadishu nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilenga mkahawa maarufu katika mji huo mkuu.

Gari dogo lililokuwa limetegwa bomu lilipuka lakini pia magaidi hao kuwapiga risasi baadhi ya watu waliokuwa ndani ya mkahawa huo.

Abdi Bashir afisa wa usalama nchini humo amesema magaidi hao watano waliwazuia watu ndani na Mkahawa huo na kuanza kuwapiga risasi lakini wakalemewa.

Aidha amesema kuwa walifanikiwa kudhibiti mkahawa huo na kuwauwa magaidi watano.

“Tunadhibiti mkahawa na tumefanikiwa kumdhibiti mshambulizi huyu wa kujitoa mhanga,” ameimbia Reuters kupitia njia ya simu.

Kundi la Al Shabab, limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Hii sio mara ya kwanza kwa mashambulizi kama haya kulenga mikahawa na maeneo mengine ya burudani nchini humo na kusababisha mauaji.