NIGERIA-BOKO HARAM

Boko Haram yasababisha vifo vya watu 16 jimboni Borno nchini Nigeria

Wanajeshi wa Nigeria wakipiga kambi mjini Maiduguri
Wanajeshi wa Nigeria wakipiga kambi mjini Maiduguri Photo: Stefan Heunis

Watu 16 wameuawa Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Nigeria baada ya magaidi wa kundi la Boko Haram kujilipua katika mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili limethibitishwa kutokea na Shirika la taifa la kushughulikia mizozo NEMA.

Msemaji wa Shirika hilo Abdulkadir Ibrahim amesema waliotekeleza shambulizi hilo lilitekelezwa na wanawake wawili waliokuwa wamejifunga mabomu mwilini.

Aidha, amesema kuwa miongoni mwa watu hao 16 waliopoteza maisha, ni washambuliaji hao.

Kundi la Boko Haram limeendelea kuwa tishio kwa raia wa Kaskazini mwa nchi hiyo na mataifa jirani.

Mamia ya watu wamepoteza maisha Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo tangu kuanza kwa mwaka huu.

Shambulizi la hivi karibuni lilitokea mapema mwezi huu na kusababisha vifo vya watu 11 karibu na mji wa Maiduguri.