DRC-WAASI

Jeshi la DRC lasema limewauawa waasi 25 wa Mai Mai Wilayani Beni

Wanajeshi wa serikali ya DRC wakikabiliana na waasi wa Mai Mai Mashariki mwa nchi hiyo wakisaidiwa na wale wa MONUSCO
Wanajeshi wa serikali ya DRC wakikabiliana na waasi wa Mai Mai Mashariki mwa nchi hiyo wakisaidiwa na wale wa MONUSCO Photo MONUSCO/Force

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema limewauwa waasi 25 wa Mai Mai baada ya mapigano yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita Wilayani Beni.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji haya yemekuja baada ya watu 13 kupoteza maisha, waasi wa Mai Mai 12 na mwanajeshi mmoja katika makabiliano hayo ya kudhibiti eneo la Kabasha.

Wakati uo huo, kundi lisilofahamika la waasi linalojiita Vuguvugu la kitaifa kla mapinduzi MNR, linadai kuwa ndilo lililokabiliana na wanajeshi wa serikali mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vofo vya watu zaidi ya 10.

John Mangaiko ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa wao ndio waliohusika na makabiliano hayo wala sio waasi wa Mai Mai kama inavyoripotiwa.

Kundi hili linasema linapigana na serikali ya Joseph Kabila.