DRC-KANISA KATOLIKI-KASAI

Kanisa Katoliki nchini DRC lasema watu 3,383 wameuawa jimboni Kasai

Ramani inayoonesha jimbo la Kasai nchini DRC
Ramani inayoonesha jimbo la Kasai nchini DRC Wikimedia Commons

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema watu 3,383 wameuawa katika jimbo la Kasai katika jimbo la Kasai tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Habari la Uingereza la Reuters, limeripoti kuwa takwimu hizo zimepatikana baada ya utafiti wa Kanisa hilo.

Ripoti hii inakuja baada ya Umoja wa Mataifa nao kusema kuwa watu waliopoteza maisha katika kipindi hicho ni zaidi ya 400 baada ya makaburi 20 ya halaiki kugundulika katika jimbo hilo.

Utafiti wa Kanisa Katoliki pia umebaini kuwa vijiji 10 vimeteketezwa moto katika jimbo hilo.

Waasi wa Kamwina Nsapu wamekuwa wakikabiliana na wanajeshi wa serikali katika jimbo hilo.

Maelfu ya watu katika jimbo hilo wameyakimbia makwao huku wengine wakikimbilia nchi jirani ya Angola.