CAR-USALAMA

Mkataba wa amani nchini CAR wasainiwa Roma

Rais wa Jumuiya ya Sant'Egidio Marco Impagliazzo (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Charles Armel Doubane, wakiwahutubia wawakilishi wa makundi yalitia saini kwenye mkataba wa amani, mjini Roma, Juni 19, 2017.
Rais wa Jumuiya ya Sant'Egidio Marco Impagliazzo (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Charles Armel Doubane, wakiwahutubia wawakilishi wa makundi yalitia saini kwenye mkataba wa amani, mjini Roma, Juni 19, 2017. FILIPPO MONTEFORTE / AFP

Serikali Jamhuri ya Afrika ya Kati ilisaini Jumatatu, Juni 19, mjini Roma, mkataba wa amani na makundi yenye silaha nchini humo chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Sant'Egidio. Majadiliano yalianza mwezi Novemba 2016.

Matangazo ya kibiashara

Makundi kumi na nne yenye silaha yaliahidi haraka kusitisha mapigano katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, "chini ya udhibiti wa jumuiya ya kimataifa". Mkataba ambao umetajwa kuwa wa "kihistoria".

Makubaliano haya yenye kurasa 16 ni "matunda ya muda mrefu, magumu na ya kweli, yalioanza mwezi Novemba 2016", alisema Maoro Garafalo. "Wananci wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waamechoka, makundi ya waasi pia," ameongeza Bw garafalo.

Mkataba huu wa amani unazungumzia kusitishwa haraka kwa mapigano. Hata hivyo hakuna muda uliotolewa kuhusu makundi ya waasi kukabidhi silaha, lakini jumuiya ya Sant'Egidio inaamini kuwa jambo hilo litatendeka haraka iwezekanavyo.

Tuna uhakika kwamba mkataba huu utachangia mchakato wa kuwaunganisha wananchi na kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia au kuwaingiza katika jeshi na polisi, kwa sababu nchi na wananchi tumechoka, amesema Mauro Garafalo, Afisa anaehusika na maswala ya Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Sant'Egidio.

Makundi ya waasi yanatambua serikali iliopo madarakani, kwa makundi haya yanaahidi kusalimisha silaha katika miezi ijayo, na baadhi ya waiganaji wataingizwa katika vyombo vya usalama na ulinzi na wengine kurejeshwa katika maisha ya kawaida, hilo ni moja la makubaliano yalioafikiwa na kutiwa saini mjini Roma.

Kwa upande wake, serikali itawajibika kutafuta uwakilishi wa makundi ya kijeshi, katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja ya ujenzi wa nchi hiyo.

Pande zote katika makubaliano hayo zimeafikiana "kufungua upya nchini humo usafirishaji huru wa watu na bidhaa na kuondolewa kwa vizuizi haramu kama matokeo ya haraka ya kusitisha mapigano," hati ya makubaliano hayo imeeleza.

Kamati ya ufuatiliaji inayoundwa na serikali, makundi yenye silaha na jumuiya ya kimataifa watahakikisha mchakato wa amani unamalizika bila tatizo lolote.