SOMALIA

Mwanajeshi aliyemuua Waziri nchini Somalia kuuawa kwa kupigwa risasi

Marehemu Waziri Abbas Abdullahi Sheikh Siraji akiwa amebebwa baada ya kuuawa mwezi Mei 2017
Marehemu Waziri Abbas Abdullahi Sheikh Siraji akiwa amebebwa baada ya kuuawa mwezi Mei 2017 REUTERS

Mwanajeshi wa Somali aliyemuua kwa kumpiga risasi Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini humo mwezi uliopita, amepewa adhabu ya kifo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Abas Abdullahi Siraji alikuwa ndani ya gari lake, karibu na Ikulu ya Mogadishu aliposhambuliwa na mwanajeshi huyo Ahmed Abdullahi Abdi.

Alipohojiwa, mwanajeshi huyo alisema alifikiri kuwa Waziri huyo alikuwa gaidi na kuamua kumpiga risasi.

Mahakama ya kijeshi iliyotoa adhabu hiyo imesema mwanajeshi huyo anaweza kukata rufaa.

Somalia bado inatekeleza adhabu na kifo kwa kupigwa risasi hadharani na kikosi maalum.

Maafisa wa juu wa serikalini nchini humo hulindwa na idadi kubwa ya walinzi waliojihami kwa silaha nzito kwa hofu ya kushambuliwa na kundi la Al Shabab.