UN-JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-CONGO

Guterres: Hatima ya wanajeshi wa Congo Brazaville kufahamika hivi karibuni

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Wikipedia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anazungumza na serikali ya Congo Brazaville kuhusu hatima ya  wanajeshi wa nchi hiyo wanaohudumu katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, MINUSCA nchini Jmahuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema wanajeshi wa Congo Brazavile wapatao  629 watarudishwa nyumbani baada ya kubainika kuhusika katika unyanyasaji wa kingono, ufisadi na kukosa nidhamu.

Gutters alitarajiwa kutangaza kuondolewa kwa wanajeshi hao nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini hatua hiyo imesitishwa ili kuruhusu mazungumzo kati yake na serikali ya Congo-Brazaville.

Awali, Kamanda wa MINUSCA Luteni Jenerali Balla Keita alikuwa ameionya serikali ya Brazaville kuwarudisha nyumbani wanajeshi wake la sivyo, umoja wa Mataifa utachukua hatua.

Mwaka uliopita, wanajeshi wengine 120 kutoka Congo Brazaville walirudishwa nyumbani kwa makosa hayo ya unyanyasaji wa kingono hasa kwa watoto.

Congo Brazaville imetuma wanajeshi 629 kusaidiana na wengine katika kulinda amani nchini humo na kituo chao kimekuwa ni Berberati, mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo.

Umoja wa Mataifa umetuma kikosi cha wanajeshi 12, 000 kulinda amani nchini