SAHEL-UNSC-UGAIDI-USALAMA

UNSC kupiga kura azimio la kutumwa kwa vikosi Sahel

Azimio la kupelekwa kwa kikosi kitakachopambana dhidi ya ugaidi kupigiwa kura na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano hii, 21 Juni.
Azimio la kupelekwa kwa kikosi kitakachopambana dhidi ya ugaidi kupigiwa kura na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano hii, 21 Juni. Manuel ELIAS / SC Chamber / AFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kupiga kura Jumatano hii asubuhi katika mji wa New York azimio linaloruhusu kupelekwa kwa vikosi vya kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel.

Matangazo ya kibiashara

Washington ilikua ilipinga kupasisha sheria yoyote aua azimio lolote la kutumwa kwa vikosi hivyo katika eneo hilo. Lakini Ufaransa, ambayo ilipendekeza hoja hiyo na Marekani hatimaye walifikia makubaliano.

Rasimu hii itakayopigiwa kura ni nakala ya makubaliano ambayo inaruhusu Ufaransa kupata msaada kutoka Marekani wakati ambapo Marekani ilikua ilipinga wazo lolote la azimio hilo.

Hata hivyo azimio hilo linabaini kwamba haliidhinisha kikosi kinachopambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel (G5) lakini tu kukubali kupelekwa kwake. Mabadiliko haya yanaihakikishia Marekani ambayo hahaitaki kupitisha kwa Umpja wa Mataifa kikosi hiki kutoka Afrika. Sura ya 7, ambayo inaruhusu matumizi ya nguvu imetoweka katika toleo hili jipya.

Amani na usalama

Marekani pia imeomba kuondolewa kwa ibara inayozungumzia kuwa ni kikosi kinachopambana dhidi ya ugaidi, kulingana na maneno yaliyoandikwa kwenye azimio hili jipya kikosi hiki kitahusika na kurejesha amani na usalama katika eneo la Sahel.

Nchini ambazo zinaunda kikosi hiki ni Mali, Niger, Chad, Mauritania na Burkina Faso, tayari zilijikubalisha kupambana dhidi ya ugaidi katika ardhi zao.

Kiwango cha fedha hakitoshi

Hatimaye, kwa upande wa fedha, bado kunatatizo, kwani kiwango cha fedha zilizokubaliwa kutolewa na Umoj awa Ulaya hakitoshi. Umoja wa Ulaya uliahidi kutoa euro milioni 5o. Fedha hizi hazitoshi kwa kupeleka askari 5000 ambao wataunda kikosi hiki.