CAR-USALAMA-MAUAJI

Watu kadhaa wauawa katika mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati

Askari wa Ufaransa wa kikosi cha opereshini Sangaris wakipiga doria katika mji wa Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Aprili 2014.
Askari wa Ufaransa wa kikosi cha opereshini Sangaris wakipiga doria katika mji wa Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Aprili 2014. © AFP PHOTO / MIGUEL MEDINA

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinaadamu yamebaini kwamba watu zaidi ya arobaini wameuawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, siku moja tu baada ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali na vikundi vya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Katiya ulitiwa saini mjini Roma, nchini Italia ukijumuisha usitishwaji mapema wa mapigano. Mkataba huo ulikua na lengo la kufikia mwisho wa mapigano yaliyodumu miaka kadhaa yakihusisha vurugu kati ya wanamgambo wa Kikristo na Waislam.

Mapema wiki hii mapigano makubwa yalitokea katika mji wa Bria, ulioko kaskazini mwa mji mkuu, Bangui.

Meya, wa mji wa Bria Maurice Belikoussou, alisikika akizungumzia kuhusu maiti za watu zilizotapakaa katika mitaa mbalimbali ya mji huo siku moja tu baada ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali na vikundi vya waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kukumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kasa makundi mawili hasimu Anti-balaka na Seleka, yanayodai kila upande kulinda jamii yake.