SUDAN-AJALI

Askari wanne wapoteza maisha katika ajali ya ndege nchini Sudan

Mji wa Khartoum, nchini Sudan.
Mji wa Khartoum, nchini Sudan. Getty Images/ Robert Caputo

Ndege ya kijeshi ya Sudan imeanguka Kaskazini mwa nchi hiyo na kuwauwa wanajeshi wanne waliokuwa ndani. Mpaka sasa jeshi linabaini kwamba ndege hiyo imeanguka kutokana na hali mbaya ya hewa.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Ahmed Khalifa Shami amesema chanzo ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa.

Mbali na hali mbaya ya hewa, makundi ya waasi yamekuwa yakihusishwa sana na uangushaji wa ndege za kijeshi katika maeneo yenye vita nchini humo.

Ajali kama hizo zimekua zikitokea nchini Sudan, huku baadhi ya vyanzo vya usalama vikidai kuwa zimekua zikisababishwa na hali mbaya ya hewa, wakati vyanzo vingine vikibaini kwamba ndege nyingi nchini humo zimekua zikidunguliwa na makundi ya waasi.