SAHEL-UNSC-UGAIDI-USALAMA

UNSC yakubali kutumwa kikosi katika eneo la Sahel

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja azimio la kupelekwa kikosi cha kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel (G5 Sahel) Jumatano Juni 21 Picha ya zamani).
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja azimio la kupelekwa kikosi cha kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel (G5 Sahel) Jumatano Juni 21 Picha ya zamani). REUTERS/Shannon Stapleton

Baada ya siku 15 za mazungumzo magumu, hatimaye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha siku ya Jumatano azimio la kupelekwa kwa kikosi cha kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel.

Matangazo ya kibiashara

Msaada huu wa kisiasa umewafurahisha wanachama wa Afrika na Ufaransa, ambayo ilipendekeza azimio hilo, lakini bado limesalia suala la fedha ambalo Marekani imeendelea kupinga.

Baraza la Usalama la limeshikamana kwa kupitisha kwa kauli moja azimio hilo, baada ya kuishawishi Marekani ambayo ilikua ikipinga kupigia kura azimio la kupelekwa kwa askari kutoka mataifa matano jirani ya ukanda wa Afrika Magharibi katika eneo la Sahel. Kikosi hiki (G5 Sahel) kimepata uungwaji mkono wa kisiasa na kisheria ambao umemridhisha Balozi wa Mali kwenye Umoja wa Mataifa Issa Konfourou.

"Kikosi hiki cha G5 Sahel, mara baada ya kutumwa huko, kitakua na kazi kubwa ya kupambana dhidi ya ugaidi, kupambana dhidi ya kuzorota kwa usalama katika eneo hilo na hali hiyo itachangia kwa usalama na amani ulimwenguni yaani tulihitajika azimio hili, " alisema Balozi Issa Konfourou.

Lakini msaada huu bado una walakini kwa sababu suala la fedha zitakazotumiwa na kikosi hiki limrtumwa kwa wafadhili wa mpango huu. "Tunajua kwamba vita hivi ni vyetu, na marais wetu wameamua kuwa katika mstari wa mbele kwa kuweka juhudi zao na uwezo wao pamoja, Balozi Issa Konfourou ameendelea . Ndiyo, tunahitaji msaada wa kimataifa. Haraka tutawasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kujaribu kuona ni katika hatua gani ambazo tunaweza kuandaa mkutano huu wa kimataifa. "

Hii ni hatua ya pili na Waafrika kama nchi za Magharibi wanatazamia kuikumbusha Marekani kwamba wamekubali kupitisha kupelekwa kwa kikosi hiki.