DRC-UN-UCHUNGUZI

DRC kuwezeshwa kiufundi katika uchunguzi wa mauaji ya Kasai

Nyumba iliobomolewa ya kiongozi wa kimila Kamuina Nsapu katika kijiji kilichopewa jina la kiongozi huyo. Nyumba hii ilibomolewa baada ya mashambulizi ya jeshi yaliosababisha kifo chake mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka jana.
Nyumba iliobomolewa ya kiongozi wa kimila Kamuina Nsapu katika kijiji kilichopewa jina la kiongozi huyo. Nyumba hii ilibomolewa baada ya mashambulizi ya jeshi yaliosababisha kifo chake mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka jana. RFI/Sonia Rolley

Wajumbe 47 wa Mataifa yanayounda Baraza la Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wameafikiana na serikali ya Kinshasa kutounda tume ya kimataifa, kuchunguza mauaji ya Kasai lakini Kinshasa itawezeshwa kiufundi kwa ajili ya kuendesha uchunguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adama Diang ambae yupo ziarani nchini DRC akisisitiza kuanzisha uchunguzi huo.

Serikali ya Kinshasa imekua ikilaumiwa kufuatia mauaji yaliyotokea katika mkoa wa Grand Kasai, wakati ambapo serikali hiyo kupitia waziri wa habari na msemaji wa serikali Lambert Mende ameendelea kulaumu mashirika yasio kuwa ya kiserikali na baadhi ya mataifa ya Magharibi kuchochea vurugu nchini DRC.

Hivi katibuni video ya mauaji hayo iliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha watau waliovalia sare za jeshi la DRC wakitekeleza mauaji dhidi ya wafuasi wa kiongozi wa kimila Kamuina Nsapu.

Awali msemaji wa serikali ya DRC Lambert Mende alikanusha video hiyo akisema kwamba ilitengenezwa kwa kuipaka tope serikali yake. Lakini siku chache baadae alibaini kwamba askari kadhaa waliohusika na mauaji walikamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.