BOTSWANA

Botswana yaomboleza kifo cha Ketumile Masire kwa siku 3

Raisi wa zamani wa Botswana Kitumile Masire
Raisi wa zamani wa Botswana Kitumile Masire DR

Rais wa zamani wa Botswana Sir Ketumile Masire, rais wa pili wa taifa hilo baada ya uhuru na ambaye aliongoza juhudi za kuleta amani kwa Msumbiji, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.

Matangazo ya kibiashara

Raisi wa Botswana Ian Khama ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha kiongozi wa zamani wa taifa hilo ambaye mazishi yake yamepangwa kufanyika Kanye kusini magharibi mwa Gaborone.

Masire alihusika sana katika jitihada za kukomesha vurugu kati ya serikali ya Msumbiji na chama kikuu cha upinzani cha Renamo katika nafasi yake kama mwenyekiti mwenza wa kundi la kimataifa la wapatanishi.

Chama cha Renamo, ambacho kilisababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 16 ambayo ilimalizika mwaka 1992, kilikataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2014 wakati kilipoangushwa na chama cha Frelimo, na kusababisha mapigano kutokea nchini kote mwaka jana.