DRC

UN yaitaka DRC kupunguza wanajeshi wake mkoani Kasai

Wanajeshi wa jeshi la DRC wakijiandaa kuingia kwenye uwanja wa mapambano
Wanajeshi wa jeshi la DRC wakijiandaa kuingia kwenye uwanja wa mapambano Reuters

Mshauri maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Adama Dieng jana Jumamosi amezihimiza mamlaka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kupunguza wanajeshi wake katika mkoa wa Kasai, baada ya kuibuka kwa vurugu mbaya za mauaji katika miezi ya hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 3,300 wameuawa katika miezi minane ya kuongezeka kwa machafuko katika mkoa wa Kasai katikati mwa DR Congo, na Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa ulisema kuwa utatuma timu ya wataalam kuchunguza ukiukwaji mkubwa wa haki katika mkoa huo.

 

Dieng ambaye nimshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauaji ya kimbari amewaambia waandishi wa habari mjini Kishasa kuwa ni muhimu kupunguza wanajeshi wa serikali mkoani Kasai na kutoa kipaumbele kwa mazungumzo baina ya pande zote mbili zinazohusika katika mzozo.

 

Aidha ameongeza kuwa hakuna maujai ya Kimbari Kasai lakini kuna vurugu zinazohitaji kukomeshwa haraka iwezekanavyo.

 

Kauli hii inakuja wakati huu wasanii wanne wa uchoraji ambao nyuo zao zilikuwa zimefunikwa kwa michoro ya rangi nyekundu kukamatwa siku ya Ijumaa mjini Goma , baada ya kuandamana kupinga kujirudia kwa mauaji mjini Beni na Kasai.

 

Mkoa wa Kasai ulipoteza utulivu baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kikabila ambaye alikuwa anapambana na serikali ya rais Joseph Kabila, wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama mwezi Agosti mwaka 2016.