CHAD-NIGERIA-BOKO HARAM

Boko Haram wawauwa wanajeshi nane wa Chad

Wanamgambo wa Boko Haram
Wanamgambo wa Boko Haram pmnewsnigeria

Wanajeshi nane wa Chad wameuawa katika mapigano makali kati ya kundi la kigaidi la Boko Haram katika kisiwa cha Ziwa Chad.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Chad Kanali Azem amesema wanjeshi wengine 18 wamejeruhiwa katika makabiliano hayo.

Aidha, amesema kuwa, wanajeshi wa Chad walifanikiwa kuwauwa wanamgambo 162 wa Boko Haram.

Chad ni miongoni mwa mataifa matano pamoja na Nigeria, Cameroon, Niger na Benin katika vita dhidi ya Boko Haram.

Chimbuko la kundi hili ni Kaskazini mwa Nigeria lakini miaka ya hivi karibuni, limeingia katika nchi jirani na kusababisha mauaji kwa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi.

Kundi hili lililoanza kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanajeshi na raia wa nchi hiyo Kaskazini mwa nchi ya Nigeria, siku ya Jumatatu limewauwa watu 13 katika mji wa Maiduguri.