NIGERIA

Rais Buhari atuma salamu za Eid kwa raia wa Nigeria

Rais wa Nigeria Muhamadu Bubari amesikika kwa mara ya kwanza, karibu miezi miwili tangu alipokwenda nchini Uingereza kupata matibabu.

Rais Nigeria Muhamadu Buhari
Rais Nigeria Muhamadu Buhari rfi Hausa
Matangazo ya kibiashara

Buhari ametuma salamu za Eid kwa raia wa Nigeria na kuwataka kuendelea kuishi na kudumisha amani nchini humo.

“Nawaomba raia wote wa Nigeria kuacha kutoa matamshi au kufanya vitendo vinavyoendelea kuharibu amani. Tuamue kuishi kwa amani,” amesema rais Buhari.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 ameendelea kupokea matibabu jijini London lakini haijaelezwa ni ugonjwa upi unaomsumbua.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikiwaambia raia wake kuwa rais Buhari anaendelea vema na hivi karibuni atarejea nyumbani.