CONGO-BRAZZAVILLE

Ufaransa yamchunguza bintiye rais wa Congo Brazzaville, Denis Sassou Nguesso

Rais wa Congo Brazzaville Dennis Sassou Nguesso
Rais wa Congo Brazzaville Dennis Sassou Nguesso REUTERS/Anis Mili

Wachunguzi nchini Ufaransa wameendeleza uchunguzi dhidi ya mali inayomilikiwa na Julienne Sassou Nguesso, binti wa rais wa Congo Brazzaville, Denis Sassou Nguesso.

Matangazo ya kibiashara

Julienne na mumewe Guy Johnson wanachunguzwa kwa madai ya kuhusika na biashara haramu ya fedha na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Wachunguzi nchini Ufaransa wanachunguza kubaini ni vipi Julienne na mumewe walivyoweza kununua jumbala kifahari lenye thamani ya Euro Milioni 3 mwaka 2006.

Inadaiwa kuwa, utajiri wa mtoto huo wa rais Nguesso unatokana na wizi wa fedha za umma kupitia ufisadi, zilizotolewa kutoka jijni Brazaville na kuhifadhiwa katika akaunti za kibinafsi nchini Ushelisheli, Mauritius na Hong Kong.

Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na wakili wa rais Nguesso, Jean-Marie Viala.