ZAMBIA-UPINZANI

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia asema anaendelea vizuri kizuizini

Hakainde Hichilema akiwa ndani ya gari wakati akienda Mahakamani jijini Lusaka
Hakainde Hichilema akiwa ndani ya gari wakati akienda Mahakamani jijini Lusaka Photo: Dawood Salim/AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, anayeendelea kuzuiliwa jijini Lusaka kwa makosa ya uhaini, amesema anaendelea vema kuzuizini.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Hichilema amewaambia wafuasi wake kuwa yeye pamoja na wenzake wanaozuiliwa wapo katika hali nzuri licha ya jitihada zinazoendelea kuwafanya wakate tamaa.

Aidha, amesema anachotaka ni ukweli ubainike Mahakamani na kuongeza kuwa wanachofanya ni kupigania demokrasia nchini mwao.

“Tunachotaka ni ukweli kufahamika Mahakakani. Lakini pia tunapigania demokrasia bora nchini Zambia kwa kila mmoja,”aliandika katika ukurasa wake wa facebook.

Mwanasiasa huyo alikamatwa na ku kufunguliwa mashtaka miezi miwili iliyopita, baada ya kutuhumiwa kuzuia masafara wa rais Edgar Lungu madai ambayo ameyakanusha.

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka uliopita, ambao Lungu alitangazwa mshindi, Hichilema alidai kuibiwa kura na hivyo kukataa kumtambua kama kiongozi wa nchi hiyo.

Serikali ya rais Lungu imekuwa ikituhumiwa kuminya demokrasia nchini humo na haki za wapinzani kujieleza.