ZIMBABWE

Mhubiri maarufu nchini Zimbabwe ashtakiwa kwa kuwachochea wanafunzi

Mhubiri Evan Mawarire akiwa Mahakamani jijini Harare Juni 28 2017
Mhubiri Evan Mawarire akiwa Mahakamani jijini Harare Juni 28 2017 REUTERS

Mhubiri maarufu nchini Zimbawe aliyeasisi maandamano dhidi ya rais Robert Mugabe mwaka uliopita, amefikishwa Mahakamani kujibu mashtaka ya uchochezi.

Matangazo ya kibiashara

Wakili wa Mhubiri huyo Evan Mawarire, amesema mteja wake alikamatwa siku ya Jumatatu na maafisa wa Polisi akiwahotubia wanafunzi wa Udaktari waliokuwa wanaandamana  kulalamikia nyongeza ya ada ya chuo.

Mhubiri huyo amefunguliwa mashtaka ya kushiriki katika mkutano usio halali na kusababisha usumbufu, madai ambayo ameyakanusha.

Ikiwa atapatikana kutekeleza kosa hilo, atahukumiwa jela miaka 10 au kulipa faini.

Hii so mara ya kwanza kwa Mhubiri huyu kufunguliwa mashtaka kama haya na baadaye kuachiliwa huru kwa ukosefu wa ushahidi.

Mwezi Julai, alikamatwa kwa uchochezi na kuandaa maandamano dhidi ya rais Robert Mugabe na kesi yake inatarajiwa kusikilizwa mwezi Septemba.