UN-USALAMA

Bajeti ya shughuli za kulinda amani za UN kuelekea kushuka

Tume za Umoja  wa Mataifa haziwezi kutekeleza majukumu yao kwa kikamilifu, wakati ambapo idadi ya askari itapunguzwa.
Tume za Umoja wa Mataifa haziwezi kutekeleza majukumu yao kwa kikamilifu, wakati ambapo idadi ya askari itapunguzwa. Communication/Nations unies

Baada ya tishio la shutdown kuendelea kushuhudiwa katika nchi mbalimbali duniani, hatimaye makubaliano yalifikiwa kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa. Bajeti ya shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa itapunguzwa kutoka Dola milioni 600 kwa jumla ya bajeti ya Dola bilioni 7.3.

Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo haya yametolewa na utawala wa Donald Trump na makubaliano hayo yatapitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.Tume zote za Umoja wa Mataifa zitathirika na upungufu huo wa bajeti, baadhi zaidi kuliko nyingine.

Marekani ilitoa pendekezo la kupunguza bajeti ya shughuli za kulinda amani Amani, suala ambalo Marekani ilikua ikitoa kama sharti la kuendelea kutoa mchango wake katika shughuli hizo za Umoja wa Mataifa. Lakini kwenye Dola milioni 600 iliyopunguzwa, theluthi tatu ni kutokana na kufungwa kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, uamuzi uliotarajiwa kwa muda mrefu.

Wanadiplomasia wanahakikisha kwamba kupunguka kwa bajeti ya shughuli za kulinda Amani ni hakikisho kuwa kuna maendeleo chanya katika shughuli za kulinda Amani duniani, lakini athari zitakuakubwa kwa tume tatu za Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na MONUSCO nchini DR Congo ambayo itapoteza Dola milioni 92, UNAMID katika jimbo la Darfur ambayo itajikuta imepungukiwa na Dola milioni 60 pamoja na Sudan Kusini ambapo tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo inatumia bajeti ilio chini ya Dola milioni 100.

Tume hizi mbili za Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na katika jimbo la Darfur zitapungukiwa na idadi ya askari wake, licha ya kuwa hali ya usalama bado tete. Wanadiplomasia wanabaini kwamba hali hiyo haitaleta madhara kwenye shughuli za tume hizo za Umoja wa Mataifa, laikini wataalamu wanasema, hata hivyo, kwamba kutakuwa na chaguo la kufanya na kwamba tume hizo haziwezi kutekeleza majukumu yao kwa kikamilifu, wakati ambapo idadi ya askari itapunguzwa.