MAREKANI-SUDAN-VIKWAZO

Marekani yatathmini kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan

Omar al-Bashir rais wa Sudan, ambayo inakabiliwa na vikwazo vya Marekani.
Omar al-Bashir rais wa Sudan, ambayo inakabiliwa na vikwazo vya Marekani. Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah

Rais wa Marekani Donald Trump ameamua kuongeza muda wa miezi mitatu zaidi wa makataa ya kuamua ikiwa nchi yake iondoe vikwazo dhidi ya Serikali ya Sudan au la, ikisema inahitaji muda zaidi kufanya mapitio.

Matangazo ya kibiashara

Hii leo Serikali ya Marekani ilikuwa iamue kuhusu hatma ya vikwazo ilivyokuwa imeiwekea nchi ya Sudan baada ya mwezi Januari mwaka huu mtangulizi wake rais Barack Obama kulegeza baadhi ya vikwazo.

Trump amesema serikali yake itafanya uamuzi huo kufikia tarehe 12 mwezi Oktoba.

Marekani inaichukulia Sudan kama nchi inayoendelea kuvunja haki za binadamu na ni moja ya nchi ambayo Marekani ilikua ikiituhumu kusaidia ugaidi duniani.