DRC

Makasisi mawili wa Kanisa Katoliki watekwa Mashariki mwa DRC

Waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo irinnews.org

Waasi wamewateka Makasisi wawili wa Kanisa Katoliki katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa Makasisi hao wanatokea katika kabila la Nande ambalo mara kwa mara limekuwa likizozana na kukabiliana na lile la Hunde.

Majina ya Makasisi hao yametajwa kuwa Charles Kipasa na Jean-Pierre Akili waliotekwa na waasi wa Mai Mai na inaaminiwa kuwa wamepelekwa milimani.

Askofu wa jimbo la Beni-Butembo Bishop Paluku Sikuli amesema pamoja na kutekwa kwa Makasisi hao, waasi hao wamechukua magari mawili na pikipiki mbili.

Waasi wa Mai Mai wamekuwa wakitekeleza utekaji nyara huu kudai kikombozi cha Mamilioni ya Dola za Marekani kuendeleza shughuli zao.

Mwaka 2012, Makasisi watatu waliotekwa karibu na mji wa Beni na waasi kutoka nchini Uganda wa ADF-NALU na inaaminiwa kuwa walipelekwa nchini Uganda na hadi leo hakuna anayefahamu waliko.