ICC-COTE D'IVOIRE-HAKI

ICC kujadili kuhusu kuachiwa kwa dhamana kwa Laurent Gbagbo

Aliekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, tarehe 28 Januari 2016, alipokua akisikilizwa kwenye Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu mjini Hague (Uholanzi).
Aliekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, tarehe 28 Januari 2016, alipokua akisikilizwa kwenye Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu mjini Hague (Uholanzi). ICC-CPI

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC inatazamia kujadili uwezekano wa kuachiwa huru kwa dhamana kwa aliekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo anaezuiliwa mjini Hague.

Matangazo ya kibiashara

Wanasheria wa kiongozi huyo wa zamani wa Cote d' Ivoire tayari wamewasilisha maombi 11 ya kutaka kuachiwa kwa Laurent Gbagbo kwa kipindi cha miaka kumi na moja na nusu, maombi ambayo yamefutiliwa mbali na mahakama. Lakini mnano mwezi Machi, baada ya kukataliwa kwa ombi la kumi na moja, wanasheria wa Gbagbo waliamua kuwasilisha ombi lao mbele ya Mahakama ya Rufaa. Mahakama ya Rufaa inatazamia kutoa uamuzi wake Jumatano hii Julai 19 alaasiri.

Mpaka sasa, ICC inatoa hoja ya mtuhumiwa huyo kuendelea kusalia kizuizini kwa Laurent Gbagbo, kwa kuhofia kuwa iwapo ataachiwa huru huenda akatoweka, kwa sababu anamtandao mkubwa ambao unaweza kuandaa kutoroka kwake. Laurent Gbagbo anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Lakini kwa upande wa utetezi, wanasema hoja hizo hazina msingii. Katika rufaa yao, wanasheria wa Laurent Gbagbo wanaishtumu mahakama kwamba haijaonyesha ushahidi wowote madhubuti wa kuwepo kwa mpango wa kutoroka na kubaini kwamba wateja wao anashikiliwa "kizuizini tu kwa kuwa ana umaarufu mkubwa. "

Hukumu ya Mahakama ya Rufaa itatolewa Jumatano hii saa 11:30 jioni saa za Afrika Mashariki, sawa na saa 8:30 saa Abidjan.