DRC-MONUSCO-USALAMA

MONUSCO yatangaza kufunga kambi zake tano Kivu Kaskazini

Idadi ya askari na kambi za askari wa MONUSCO itapungua katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Idadi ya askari na kambi za askari wa MONUSCO itapungua katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Eduardo Soteras / AFP

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO) imefunga kambi tano miongoni mwa kambi zake mkoani Kivu Kaskazini. Kivu Kaskazini inakabiliwa na mashambulizi ya makundi mengi yenye silaha.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo imeondoa idadi ya askari wake waliotumwa katika maeneo ya Masisi na Walikale. Lakini pia katika kusini mwa Lubero, pamoja na kufungwa kwa kambi ya Luofu. Hali hii inajitokeza kufuatia kupunguzwa kwa bajeti na ombi la serikali ya DR Congo la kupunguza idadi ya vikosi vya Umoja wa Mataifanchini humo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliomba MONUSCO kupunguza askari wake 2,500. Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, uamuzi huu umesababisha karibu bataliani yote kuondoka katika maeneo hayo, sawa na askari 750 na makambi yao kufungwa.

Hakuna tena uwepo wa tume ya kudumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Walikale, ambapo bado kuna makundi mengi yenye silaha. Kundi jipya lilianzisha hivi karibuni kutokana na mgogoro kati ya wachimba migodi wa jadi na jamii ya Alphamine.

Katika eneo la Masisi pia, kambi mbili zimefungwa, uwepo wa tume ya kudumu ya Umoja wa Mataifa katika eneo hilo itapungukiwa na askari pamoja na wafanyakazi wake. Katika eneo hili, pia kuna makundi yenye silaha yanayohujumu raia, lakini hasa kwa wakati huu mapigano ya kikabila kati ya jamii ya Wahutu na Hunde.

Pia, kufungwa kwa kambi ya Luofu kusini mwa Lubero iliokumbwa na mauaji mwaka 2016, kama yale ya Miriki au Luhanga.

Kwa upande wa tume ya Umpoja wa Mataifa nchini DRC, wanahakikisha kwamba kupunguzwa huko haimaanishi kuondoka kwa MONUSCO nchini DRC na hali hii itawawezesha kupelekwa vitengo zaidi katika maeneo hatari, ikiwa ni pamoja kwenye ngome sambamba kambi zilizofungwa leo.

"Tutafanya kila tuwezalo kwa kile tulichojaliwa, unaona Bw. Trump," amesema afisa wa Umioja wa Mataifa ambaye kwa namna fulani anaamini kwamba njia pekee ya kukomesha ukosefu wa usalama katika mkoa wa Kivu Kaskazini ni kushambulia makundi yenye silaha yanayoonekana zaidi, lakini pia kwa wale wanaochangia kuhatarisha usalama huo.