Pata taarifa kuu
DRC-UN-MAUAJI

Serikali ya DRC kuhusishwa kwa mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataiafa

Rais wa DRC  Joseph Kabila ambaye, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa serikali yake inaweza kuhusishwa kwa mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa.
Rais wa DRC Joseph Kabila ambaye, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa serikali yake inaweza kuhusishwa kwa mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa. REUTERS/Kenny Katombe
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Watalaam wa Umoja wa Mataifa wanaochunga mauaji ya watalaam wa Umoja huo Michael Sharp na Zaida Catalan waliotekwa na kuuawa jimboni Kasai nchini DRC, wanasema kuna uwezekano kuwa wanajeshi wa serikali waliohusika katika mauaji hayo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya awali ya watalaam hao kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hata hivyo, haijaeleza moja kwa moja kuwa wanajeshi wa serikali walihusika wakati huu uchunguzi ukiendelea. Serikali ya Kinshasa imewashtumu waasi wa Kamwina Nsapu kuhusika katika mauaji hayo.

Wakati huo huo, maafisa wa usalama nchini humo wanasema bado hawajafanikiwa kuwapata Mapadri wawili wa Kanisa Katoliki waliotekwa na watu wasiofahamika.

Hayo yakijiri watu sita miongoni mwao waasi maimai wa mazembe na wengine wawili kutoka kundi la waasi la Nduma wameripotiwa kuuawa katika makabiliano makali kati ya jeshi la serikali ya DRC Wilayni Lubero Mashriki mwa nchi hiyo katika maeneo ya Kyambuli na Kimaka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.