DRC-UFISADI

Global Witness yadai fedha za madini zimefujwa nchini DRC

Mdogi wa maduni wa  Kibali Kaskazini Masharkiki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Mdogi wa maduni wa Kibali Kaskazini Masharkiki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Reuters

Shirika la Kimataifa linalopambana na ufisadi la Global Witness, linasema asilimia 20 ya mapato yanayopatikana kutokana na biashara katika sekta ya madini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia yanayokadiriwa kuwa Dola Milioni 750, hayajawasilishwa katika Wizara ya fedha kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Pete Jones, mmoja wa wanaharakati wa Shirika hilo, amesema fedha hizo zimefujwa na kutumiwa visivyo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali ya Kinshasa, badala ya kuwanufaisha raia wa kawaida.

Aidha, Jones amesema fedha za sekta ya madini zinatumiwa kufanya biashara na kufichwa katika benki za nje ya nchi na kuwanufaisha watu wachache.

Hata hivyo, serikali ya DRC imekuwa ikikanusha madai ya kufuja fedha kutoka katika sekta hiyo na kusisitiza kuwa madai ya Global Witness, hayana ukweli.

DRC ina utajiri mkubwa wa madini kote duniani lakini wananchi wake wanaendelea kuishi kwa umasikini mkubwa.

Utajiri wa madini umeelezwa kuwa chanzo cha utovu wa usalama Mashariki mwa nchi hiyo, eneo ambalo kuna makundi mengi ya waasi.

Raia wa DRC wameendelea kuilamu serikali kwa kushindwa kuhakikisha kuwa madini hayo yanawanufaisha.