SENEGAL-SIASA-UCHAGUZI

Matokeo ya kura yatarajiwa kutangazwa Senegal

Zoezi la Kuhesabu kura mjini Dakar, Senegal, Julai 30, 2017.
Zoezi la Kuhesabu kura mjini Dakar, Senegal, Julai 30, 2017. Guillaume Thibault/RFI

Siku moja baada ya uchaguzi nchini Senegal siku ya Jumapili, matokeo ya uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa. Uchaguzi huu wa wabunge ulifanyika katika hali ya utulivu, huku televisheni ya umma ikiripoti kuwa asilimia 54 ya raia wa nchi hiyo walijitokeza kupiga kura.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo uchaguzi huo uligubikwa na matatizo ya maandalizi, jambo ambalo sikawaida katika nchi hiyo. Lakini licha ya ucheleweshaji wa kuanza kwa uchaguzi huo, vitio vya kupigia kura vilifungwa kwa muda uliopangwa saa 12 jioni saa za kimataifa.

Uchaguzi huu ulikubigwa na matatizo mbalimbali. Ilibidi kuw na muda wa kuweka sawa vituo vya kupigia kura kwa sababu kulikua na 47 kwa uchaguzi huo. Tatizo jingine wapiga kura kadhaa waliokua na kadi ya kupiga kura walijikuta hawakuandikwa kwenue daftari la kupigia kura.

Rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade, amemshutumu rais wa sasa anae waniwa muhula mwingine, Macky Sall, kwa wizi wa kura, akisema kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa bado hayajapokea kadi za kupigia kura.

Polisi imesema wagombea watatu wa muungano wa Abdoulaye Wade walikamatwa kwa kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura.

Rais Sall anatafuta wingi wa viti katika chama chake.

Abdoulaye Wade amethibitisha kuwa muunngano wa vyama vidogo vidogo unamuandaa mtoto wake wa kiume Karim kuwania urais mnamo mwaka 2019.

Itafahamika kwamba kuna mgombea mwingine ambaye ni meya wa mji mkuu wa Senegal, Dakar, yukojela kwa mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya umma.