DRC-USALAMA

Mvutano wa kisiasa waendelea kushuhudiwa DRC

Jamhuri ya Kideokrasia ya Congo yaendelea kukumbwa na mvutano wa kisiasa
Jamhuri ya Kideokrasia ya Congo yaendelea kukumbwa na mvutano wa kisiasa Reuters/ File

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama, Basile Olongo, imesema kuwa hali ya usalama ni tulivu katika miji kadhaa iliyoshuhudia makabilianao makali kati ya jeshi la polisi na waandamanaji, siku ya Jumatatu katika nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Bw Olongo amesema maandamano yaliyoandaliwa na vuguvugu la vijana linalopigania mabadiliko, demokrasia na uongozi bora LUCHA yalikuwa yamepigwa marufuku na serikali.

Wanaharakati hawa wanasema maandamano yao yalikuwa yenye lengo la kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi mwaka huu, lakini pia kupinga uongozi wa rais Joseph Kabila.

Kwa upande wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila vimesema hakuna haja ya kuharakisha uchaguzi huo.

Kwa ujumla waandishi wa habari 13 Walikamatwa nchini humo, huku wakipokonywa vifaa vyao vya kazi, lakini baada ya saa mbili waliachiwa huru.