ITALI-LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Italia kukabiliana na wahamiaji wanaotokea Libya

Wanaharakati wa haki za binadamu wanahofia kuwa hatua ya Itali ya kuwazuai wa hamiaji itawafanya wahamiaji zaidi kukiuka sheria za uhamiaji ikiwa watarejeshwa Libya.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanahofia kuwa hatua ya Itali ya kuwazuai wa hamiaji itawafanya wahamiaji zaidi kukiuka sheria za uhamiaji ikiwa watarejeshwa Libya. Reuters/Stefano Rellandini

Bunge la Italia limepitisha mpango wa kutuma meli za kivita katika bahari ya Libya kuwazuia wahamiaji kutoka Libya kuvuka bahari ya Meditarenia. Itala haitaki wahamiaji na wakimbizi zaidi wanaowasili nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kura ya hivi karibuni ya bunge iliashiria mwanzo wa mafanikio ya azma ya taifa hilo kuwarudisha nyuma wahamiaji na wakimbizi katikati mwa bahari ya Mediterranean.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanahofia kuwa hatua hii ya Italia itawafanya wahamiaji zaidi kukiuka sheria za uhamiaji ikiwa watarejeshwa Libya.

Wahamiaji wanaohifadhiwa wanaishi mazingira duni, huku ikiaminika kuwa wamekua wakifanyiwa vitendo udhalili kama kupigwa na hata kubakwa.

Italia ni nchi inayopokea wahamiaji wengi wanaosafiri kutoka Libya, nchi ambayo inaaminika kuwa kitovu cha wahamiaji wengi kutoka kusini mwa jangwa la Sahara kuingia Ulaya.

Hivi karibuni wizara ya ulinzi ya Itali ilituma meli mbili ndani ya eneo la maji la Libya kusaidia walinzi wa mwambao wa Libya kukabiliana na wahamiaji wanaoelekea Ulaya kupitia Itali.