Habari RFI-Ki

MONUSCO yaitaka DRC kuheshimu haki ya kuandamana

Imechapishwa:

Baada ya Umoja wa Mataifa kuitaka serikali ya DRCongo kuheshimu haki ya raia kuandamana kama inavyoagizwa na katiba ya nchi hiyo, serikali kupitia waziri wake wa habari ambae pia ni msemaji wa serikali Lambert Mende amesema serikali inaheshimu haki ya raia kuandamana.Hii inakuja wakati huu vyombo vya Usalama nchini humo vikiwatia nguvuni watu zaidi ya 120 waliojaribu kuandamana katika miji kadhaa ya nchi hiyo, ambapo umoja wa Mataifa unasema wengi wa waliokamatwa waliachiwa huru ispokuwa watano kutoka mashirika ya kiraia mjini Lubumbashi.

Waziri wa habari nchini DRC Lambert Mende
Waziri wa habari nchini DRC Lambert Mende REUTERS/Kenny Katombe