Pata taarifa kuu
DRC-MAJANGA ASILI

DRC yathibitisha vifo vya watu 40 kufuatia maporimiko ya udongo

Barabara nyingi zimeharibika kutokana na mafuriko katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC.
Barabara nyingi zimeharibika kutokana na mafuriko katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC. RFI/Habibou Bangré
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Naibu gavana wa jimbo la Ituri Pacifique Keta amesema kuwa watu wasiopungua 40 ndio wamepoteza maisha katika maporomoko ya ardhi.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limekiharibu kijiji cha Tora wanakoishi wavuvi katika ukingo wa ziwa Albert kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo,

Bw Keta ameliambia shirika la habari la ufaransa AFP kuwa sehemu ya mlima ilifunika kambi ya wavuvi baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi

Daktari katika hospitali ya mji ulio jirani na eneo la tukio, mji wa Tshomia Herve Isamba, amesema wanawatibu watu wanne waliopata majeraha katika maporomoko hayo.

Kumekuwa na majanga mabaya ya maporomo ya ardhi mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo miaka ya hivi karibuni.

Janga hili linatokea baada ya mafuriko mabaya yaliyotekea kwenye mji wa Freetown nchini Sierra Leone siku ya Jumatatu ambayo yaliwaua watu 300.

Ripoti zinasema kuwa watu wote 40 waliopoteza maisha tayari wamezikwa

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.