Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-WAKIMBIZI-USALAMA

Mkutano mdogo kuhusu mgogoro wa wahamiaji kufanyika Ufaransa

Mjini Roma, polisi hutumia maji kwa kuzima makabiliano na wakimbizi katikati ya mji mkuu wa Italia, Agosti 24, 2017.
Mjini Roma, polisi hutumia maji kwa kuzima makabiliano na wakimbizi katikati ya mji mkuu wa Italia, Agosti 24, 2017. REUTERS/Yara Nardi
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Mkutano kuhusu wahamiaji unafunguliwa Jumatatu hii mchana kwenye ikulu ya Elysée mjini Paris nchini Ufaransa. Rais Emmanuel Macron atawapokea marais wa Chad Idriss Deby na Niger, Mahamadou Issoufou.

Matangazo ya kibiashara

Pia katika mkutano huo wamealikwa Kansela wa Ujerumani Angel Merkel, mkuu wa mashauriano ya kigeni wa Ulaya Frederica Mogherini, Waziri Mkuu wa Italia Paolo Gentiloni, Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy na kiongozi wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Fayez Al Sarraj.

Mkutano huu unafanyika wakati ambapo katika majira haya ya joto, Emmanuel Macron aliomba kuundwe barani Afrika, vituo vya usajili kwa watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi ili kupunguza wingi wa wakimbizi wanaoingia Ulaya kinyume cha sheria, vifo katika bahari Mediterranean na kuzuiliwa kikatili kwa wakimbizi nchini Libya.

Hivi karibuni rais wa Ufaransa alitangaza hadi kufikia mwaka 2018 kambi za wakimbizi zitakua zimefungwa, na kufunguliwa kwa vituo vya usajili kwawatu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi nchini Libya. Kutokana hali ya usalama nchini Ufaransa, ikulu ya Elysee ilisahihisha msimamo wake na hatimaye kutangaza kujengwa kwa vituo vya usajili kwa watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi nchini Niger na Chad.

Tunapinga mradi huu ambao unakuja kuzidisha hali ya hatari nchini. Maelfu ya wahamiaji watakimbilia hapa nchini, "amesema waziri wa mambo ya Kigeni wa Chad, Hissein Brahim Taha. Kwa mujibu wa Bw. Brahim Taha, ujumbe wa Ufaransa ulikuja mara mbili mjini Ndjamena mwezi huu. ikiwa ni pamojaa na Ofpra, taasisi ya Ulinzi kwa Wakimbizi.

"Tulizungumzia kuhusu wakimbizi 400,000 wanaoishi katika ardhi yetu. Ujumbe ulitaka kuona jinsi ya kuwasaidia kuwapatia makazi kama walikuwa na haki ya hifadhi, huku wakiwa katika mazingira magumu zaidi. Hatukuzungumzia kuhusu viituo vya usajili kwa watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi, " amesema Hissein Brahim Taha.

Wadiplomasia wa Ufaransa pia walikuja "kuona jinsi wanavyoweza kutusaidia kulinda mpaka na Libya," alisema waziri huyo.

Ni vigumu kujua kitakachotokea kataika mkutano huu wa kirafiki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.