DRC-UCHAGUZI

Zoezi la kuandikisha wapiga kura katika Kasai kuanza Septemba 4

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini DRC imesema zoezi la kuhakiki na kuandikisha wapiga kura wapya kwenye majimbo mawili ya Kasai ambako kumeshuhudiwa machafuko hivi karibuni, litaanza September 4 na kisha kuendelea kwenye majimbo mengine 24

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi CENI Corneille Nangaa  Yobeluo (kushoto).
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi CENI Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto). MONUSCO/Alain Wandimoyi
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi CENI, Corneille Nangaa amewataka wananchi kuwasaidia maofisa wake kufanya kazi kwa uhuru kuandaa uchaguzi.

Katika hatua nyingine upinzani umekosoa takwimu za hivi karibuni zilitolewa na tume hiyo ukisema kwa kiwango kikubwa haziko sawa.

CENI inasema jumla ya wapiga kura milioni 40 wameandikishwa kwenye majimbo mengine 24 huku taifa hilo likiwa na jumla ya raia milioni 70 wengi wakiwa bado hawajaandikishwa.