DRC-USALAMA

Viongozi kujaribu kurejesha amani Kasai, DRC

Jiji la Kananga, mji mkuu wa mkoa wa Kasai ya Kati, ambako kunafanyika semina kuhusu amani.
Jiji la Kananga, mji mkuu wa mkoa wa Kasai ya Kati, ambako kunafanyika semina kuhusu amani. wikipedia

Katika mji wa Kananga, nchini DRC, kumeandaliwa Jumatatu hii semina kabambe kuhusu Amani na maridhiano katika mikoa mitano ya Kasai, na hasa Kasai ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Semina hiyo ambayo inafunguliwa Jumatatu hii, Septemba 18 itaruhusu wakazi wa mikoa hiyo kuzungumza na kuweka wazi kila mmoja na kile alichohusika katika mapigano yaliyosababisha vifo vingi yaliyotokea miezi ya hivi karibuni kati ya jeshi la DR Congo na wapiganaji wa Kamuina Nsapu. Mpango ambao unaofufua shauku na mashaka.

Wakuu kimila na Wakuu wa mikoa mitano mitano ya Kasai watashiriki semina hii lakini upinzani umekataa mwaliko. Upinzani unaomba uchunguzi kabla yayote, na inataja mkutano wa sasa kama "kongamano dogo" la chama tawala cha PPRD.

Naibu Waziri Mkuu wa mambo ya ndani yuko Kananga tangu siku ya Jumapili, na baada ya kufika, Emmanuel Ramazani Shadari alitangaza jinsi semina hiyo ilivyoandaliwa.Kwa mujibu wa Bw Shadari, "kunahitajika mkutano ambapo watu wanapaswa kuzungumza, kujadili kwa pamoja, ili kuambiana ukweli, ili kukemea na kulaani kile kilichotokea katika jimbo la Kasai".

Wito wa maridhiano na amani ulitangulia mkutano huu. Wakisaidiwa na mitandao ya kijamii, viongozi kadhaa wa kisiasa na vyeo vingine katika jimbo la Grand Kasai walisisitiza umuhimu wa msamaha kabla ya maridhiano ya aina yoyote.

Msamaha Kabla ya maridhiano

"Kila kitu ambacho kinaweza kuleta amani kwa Kasai kinakaribishwa na kupongezwa. "Kwa upande wa Anaclet Tshimbalanga, mkazi wa Kasai na mtaalamu wa uratibu wa migogoro ya kimila, amesema serikali ina muelekeo mzuri. Lakini ili semina hii ifaulu, itabidi watu wenye msimamo mzuri, wadau wenye uelewa wa kuongea wapewe na fasi ya kuzungumza.

"Kinachohitajika, ni kuwapa nafasi ya kuongeza wawakilishi wa makabila yanayokabiliwa na migogoro, kwa hiyo ninafikiria wakuu wa kimila, viongozi wa vijijini ambao wamejaribiwa sana na wanaohitaji kuelezea matatizo yao halisi, "Bw Tshimbalanga amesema.

Kulingana na ripoti ya Kanisa Katoliki, vurugu katika jimbo la Kasai zimeua watu zaidi ya 3,000 na wengine zaidi ya milioni moja wametoroka makazi yao ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.