LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Zaidi ya wahamiaji 100 watoweka katika pwani ya Libya baada ya boti lao kuzama

Wahamiaji wakisubiri kuokolewa na kikosi cha wanamaji cha Italia, kilomita 30 kutoka pwani ya Libya, tarehe 6 Agosti 2017.
Wahamiaji wakisubiri kuokolewa na kikosi cha wanamaji cha Italia, kilomita 30 kutoka pwani ya Libya, tarehe 6 Agosti 2017. ANGELOS TZORTZINIS / AFP

Zaidi ya wahamiaji 100 wametoweka baada ya boti lao kuzama kusini magharibi mwa Libya, msemaji wa kikosi cha wanamaji cha Libya ameliambia shirika la habari la AFP Alhamisi hii (Septemba 21), akibaini kwamba kuna manusura waliokolewa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Jenerali Ayoub Kacem, "watu saba walionusurika" walikaa katika bahari kwa siku tatu kabla ya kuokolewa siku ya Jumatano.

Ayoub Kacem hakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu kuzama kwa boti hilo, ajali ambayo ilitokea katika pwani ya Sabratha, magharibi mwa mji wa Tripoli.

Wahamiaji 3,000 walirudishwa Libya na wengine 2,000 waliwasili Italia.

Wiki iliyopita, zaidi ya wahamiaji 3,000 walirudishwa kutoka nyuma kutoka katika bahari ya Mediterranean na kikosi cha walinzi wa pwani la Libya huku wengine 2,000 wakiendelea hadi Italia, kulingana na ripoti iliyotolewa na vyanzo kadhaa vya serikali na vyombo vya habari vya Italia.

Italia imeorodhesha wahamiaji 6,500 tangu katikati ya mwezi Julai, asilimia 15 tu ya wastani kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi mwaka 2016.

Shirika la Umoja wa Mataifa kinaloshughulikia maswala ya uhamiaji (IOM) linaripoti kwamba wahamiaji na wakimbizi 53,912 wameingia Ulaya kwa nji ya baharini mwaka 2017, ambapo watu 1,366 walikufa maji wakati walipokua wakivuka hadi Mei 14 mwaka 2017.