DRC-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano makali yaripotiwa pembezoni mwa mji wa Uvira, DRC

Mji wa Uvira, mashariki mwa DR Congo, ambapo mapigano yanaendelea kurindima kati ya waasi na jeshi la DRC.
Mji wa Uvira, mashariki mwa DR Congo, ambapo mapigano yanaendelea kurindima kati ya waasi na jeshi la DRC. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh

Milio ya silaha na zana nzito nzito za kijeshi vinaendelea kusikika pembezoni mwa mji wa Uvira, mji wa pili wa mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC. Mapigano hayo ni kati ya wapiganaji wa Mayi Mayi wa kundi la CNPSC la William Yakutumba na vikosi vya jeshi vya serikali (FARDC).

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano waasi hawakuweza kuingia katika mji huo. Vikosi vya jeshi la serikali (FARDC) viliweza kuwarejeha nyuma. Wakazi wa mji wa Uvira wameanza kuutoroka mji huo kufuatia mapigano hayo.

Maduka, shule na ofisi mbalimbali za serikali zimefungwa kwa siku ya leo katika mji huo. Hali ya utulivu ilikua ilirejea jana jioni.

kundi hili la waasi tayari limedhibiti baadhi ya maeneo mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na eneo la Mboko.

Kundi hili la waasi la CNPSC, lilianzishwa mwaka 2013 na linaongozwa na afisa wa zamani wa FARDC aliyeasi. William Amuri, almaarufu Yakutumba, ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Fizi katika mkoa wa Kivu Kusini aliondoka jeshini mwaka 2007. Leo, anasema kuwa ana wapiganaji 10,000 wanaoendesha vita sehemu mbili: moja kaskazini kuelekea Uvira, upande mwingine kusini mwa Kalemie.

Idadi hii ni kubwa, kwa mujibu wa vyanzo vya mbalimbali nchini humo, ambavyo vinabaini kwamba kundi hili lina zaidi ya wapiganaji 100, ikiwa ni pamoja na watoto.

William Yakutumba, anasem anaendesha "vita vya uhuru", kwa maneno yake mwenyewe. Uvira ni hatua moja tu katika mpango wake wa kuikomboa nchi nzima. Itachukua miezi isiozidi miwili tu kwa kuudhibiti mji wa Kinshasa na kuuangusha utawala wa Kabila, amesema Wiliam Yakutumba.

Msemaji wa FARDC, ambaye siku ya Jumatatu alielezea kundi hilo kama la "majambazi", anasema kundi hili linapata msaada kutoka pwani nyingine za Ziwa Tanganyika, Burundi au Tanzania.