DRC-UN-USALAMA

Antonio Guterres aomba Monusco kuwa na nguvu zaidi

Ujumbe wa ukaguzi uliofanywa mwaka 2016 na Monusco katika maeneo duni ya DRC.
Ujumbe wa ukaguzi uliofanywa mwaka 2016 na Monusco katika maeneo duni ya DRC. MONUSCO / Taimoor

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasilisha kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapitio yake ya kimkakati ya Monusco, tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

Bw Guterres anabaini kwamba kupunguzwa kwa bajeti iliyoamuliwa mnamo mwezi Machi mwaka 2017 kutazuia tume hii kutekeleza wajibu wake nchini humo na kuonya Mataifa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kupunguza zaidi kwa askari wa kulinda amani nchini DRC kutadhoofisha uwezo wake na kusababisha nchi hii inakumbwa machafuko kabla ya uchaguzi wenye utata.

Antonio Guterres ameomba kikosi cha Umoja wa mataifa nchini DR Congo kiimarishwe na kipewe uwezo wa kutosha haraka iwezekanavyo kwa kutekeleza majukumu yake.

Bw Guterres pia ameonya kutothubutu kupunguza bajeti ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DR COngo, wakati ambapo Monusco tayari imepunguziwa 8% ya bajeti yake na wala haitakua na uwezo wa kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo. Kwa hiyo ni muhimu kuzingatia malengo mawili yanayopewa kipaumbele: utekelezaji wa mkataba wa Desemba 31 na ulinzi wa raia.

Katibu Mkuu wa Umoja w Mataifa amesema kuwa Monusco inapasw ipewe uwezo wa kutosha na kutumwa askari wake katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Askari wa kikosi hicho wanapaswa kupelekwa kwa haraka kulingana na dharura ya usalama.

Antonio Guterres aomba Monusco kuwa na nguvu zaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres almewasilisha kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapitio yake ya kimkakati ya Monusco, tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Bw Guterres anabaini kwamba kupunguzwa kwa bajeti iliyoamuliwa mnamo mwezi Machi mwaka 2017 kutazuia tume hii kutekeleza wajibu wake nchini humo na kuonya Mataifa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, kupunguza zaidi kwa askari wa kulinda amani nchini DRC kutadhoofisha uwezo wake na kusababisha nchi hii inakumbwa machafuko kabla ya uchaguzi wenye utata.

Antonio Guterres ameomba kikosi cha Umoja wa mataifa nchini DR Congo kiimarishwe na kipewe uwezo wa kutosha haraka iwezekanavyo kwa kutekeleza majukumu yake.

Bw Guterres pia ameonya kutothubutu kupunguza bajeti ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DR COngo, wakati ambapo Monusco tayari imepunguziwa 8% ya bajeti yake na wala haitakua na uwezo wa kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo. Kwa hiyo ni muhimu kuzingatia malengo mawili yanayopewa kipaumbele: utekelezaji wa mkataba wa Desemba 31 na ulinzi wa raia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa Monusco inapasw ipewe uwezo wa kutosha na kutumwa askari wake katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Askari wa kikosi hicho wanapaswa kupelekwa kwa haraka kulingana na dharura ya usalama.