DRC-MONUSCO-USALAMA

Kambi ya Monusco yashambuliwa karibu na mji wa Beni, DRC

Askari wa Monusco, tarehe 23 Oktoba 2014, Beni..
Askari wa Monusco, tarehe 23 Oktoba 2014, Beni.. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wilaya ya Beni, katikamkoa wa Kivu Kaskazini, linashuhudia mdororo wa usalama baada ya miezi kadhaa ya utulivu.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF) wamekua wakiendesha tangu Ijumaa mashambulizi kabambe katika maeno yalitojirani ya Wilaya ya Beni, mashariki mwa DRC.

Baada ya kuua zaidi ya raia wa kawaida 30 siku mbili zilizopita, kundi hili lilishambulia mapema Jumatatu asubuhi kambi ya kikosi cha Umoja Wamataifa nchini DRC (Monusco), kilomita thelathini kutoka mji wa Beni.

 

askari mmoja wa Monusco aliuawa na wengine kumi na wawili kujeruhiwa katika shambulizi dhidi ya kambi ya Monusco inayopatikana kati ya Kamango na Mbau, kwa mujibu wa msemaji wa Monusco, Florence Marchal.

Bw. Marchal anahusisha shambulio hilo kwa kundi la waasi wa Uganda wa ADF. Amehakikisha kwamba kambi hiyo bado iko chini ya udhibiti wa jeshi la Umoja wa Mataifa. Helikopta za kijeshi pia zilitumiwa kwenyeeneo hilo.

Vyanzo vya kutoka vyama vya kiraia, vilivyohojiwa mjini Beni, vimebaini kwamba gari moja ya kivita ya Monusco imeharibiwa vibaya. Vyanzo hivyo vimeongezea kwamba waasi wa ADF walirejea nyuma kilomita zaidi ya kumi mashariki mwa DRC.

Raia wachinjwa

Mashambulizi haya yalianza siku ay Ijumaa waki ambapo ilikuwa miezi kadhaa hali ya utulivu ikishuhudiwa katika eneo. Kundi la ADF lilojihami kwa silaha za kivita liilizindua mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya ngome nne za jeshi la DRC, FARDC, katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga, mashariki mwa Beni. Askari wa DRC walifukuzwa siku moja baadaye kwenye ngome zao. Ngome amabzo zilichukuliwa miezi michache iliyopita kutoka mikononi mwa waasi hawa wa Uganda. Askari wa DRC walilazimika kukimbilia kilomita arobaini kutoka mji huo.

Kundi hili la waasi wa Uganda linaelekea mjini Beni. Mashirika ya kiraia katika eneo hili yana wasiwasi na yamekua yakijiuliza kuhusu waasi hawa wa ADF kutoka Uganda ambao wanaonekana kuwa na nguvu kubwa, huku kundi hili likiwa na wapiganaji wengi na silaha nyingi ikilinganishwa na hapo awali.