LIBERIA-UCHAGUZi-SIASA

George Weah, nyota wa soka zamani aongoza kwa kura Liberia

Mwanasoka wa zamani George Weah katika mkutano wa kampeni ya chama chake. Monrovia, Novemba 20, 2014.
Mwanasoka wa zamani George Weah katika mkutano wa kampeni ya chama chake. Monrovia, Novemba 20, 2014. AFP PHOTO / Zoom Dosso

Nchini Liberia kura zinaendelea kuhesabiwa, na tayari nyota wa zamani wa soka George Opong Weah anaongoza kwa kura, kulingana na matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mgombea anayefuatia ni makamu wa rais Joseph Boakai,ambaye anaongoza katika jimbo moja na mengine yanayosalia ameshika nafasi ya pili.

Atakayetangazwa mshindi anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Ellen Johnson Sirleaf.

Ellen Johnson Sirleaf, mshindi wa Nobel, anamaliza muda wake kwa mjibu wa katiba ya Liberia.

Takwimu kutoka tume ya uchaguzio NEC zinaonyesha Weah yupo mbele kwa majimbo 11 kati ya majimbo 15 japo zoezi la kuhesabu kura linaendelea.

Mshindi katika uchaguzi huo anatakiwa kupata 50 % ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi, na kama hakuna mgombea atakayefikisha kiwango hicho, uchaguzi wa marudio utapewa nafasi kwa muda usiozidi siku 20 yaani mnamo mwezi Novemba.

Hata hivyo duru mbili ndio zitaamua ushindi wa rais mpya wa nchi hiyo. Uchaguzi huu ni wa kihistoria ambao ambapo itakua mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe utawala unakabidhiwa kwa njia ya kidemokrasia kutoka kwa rais anayemaliza muda wake akimkabidhi rais aliyechaguliwa.

Miongoni mwa wagombea katika uchaguzi huo ni Joseph Nyumah Boakai, Charles Brumskine, Alexander Cummings, Benoni Urey na George Weah.