DRC-MONUSCO-SIASA-USLAMA

Monusco: Wanasiasa wanatakiwa kuheshimu makubaliano ya mwaka 2016

Monusco yawataka wanasiasa wa DRC kuyapa kipaumbele makubaliano ya kisiasa ya mwaka 2016.
Monusco yawataka wanasiasa wa DRC kuyapa kipaumbele makubaliano ya kisiasa ya mwaka 2016. CC/MONUSCO/Clara Padovan

Tume ya umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imewataka wanasiasa nchini humo kuheshimu makubaliano ya kisiasa ya mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yanataka uchaguzi ufanyike mwishoni mwa mwaka huu, lakini tume ya uchaguzi imesema kuwa inahitaji siku 504 kuandaa uchaguzi hatua ambayo inapingw ana wapinzani.

Wakati huo huo mapigano makali yameshuhudiwa kati ya jeshi la serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na waasi wa uganda wa kundi la ADF katika maeneo ya barabara inayounganisha miji ya Mbau na Kamango wilayani Beni, mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti zinasema kuwa waasi hao walivamia msafara wa kamanda mkuu wa operesheni ya jeshi jenerali Marcel Mbangu, na kuua askari mmoja na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa.

Kundi la waasi wa Uganda la ADF limekua likiendesha mashambulizi ya hapa na pale katika maeneo jirani ya mji wa Ben, Mashariki mwa DRC.

Watu wengi wameuawa na kundi hili na wengine wengi wamelazimika kuyahama makazi yao kwa kuhofia usalama wao.