SOMALIA-UGANDA-USHIRIKIANO-USALAMA

Rais wa Somalia ziarani Uganda

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed "Farmajo" katika mkutano wa kilele wa jumuia ya kikanda ya Igad kuhusu hali ya wakimbizi wa Somalia katika ukanda wa Afrika ya mashariki, Nairobi, Machi 25, 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed "Farmajo" katika mkutano wa kilele wa jumuia ya kikanda ya Igad kuhusu hali ya wakimbizi wa Somalia katika ukanda wa Afrika ya mashariki, Nairobi, Machi 25, 2017. SIMON MAINA / AFP

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo anazuru nchi ya Uganda kwa ziara ya kiserikali. Haijajulikana lengo la ziara hii.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inafanyika wiki moja tu baada ya shambulio baya kuwahi kutokea nchini humo tangu kundi la Al shabba kuanzisha mashambulizi yake mnamo mwaka 2007. Shambulio hili lilisababiha vifo vya watu zaidi ya 300.

Mpaka sasa lengo la safari yenyewe halijajulikana lakini duru za kuaminika zinasema ziara hii inauhusiano na usalama wa mji mkuu Mogadishu unaozidi kudorora siku baada ya siku.

Itafahamika kwamba Uganda ndio nchi ambayo ina askari wengi katika kikosi cha askari wanaosimamia usalama nchini Somalia..

Shambulio la hivi karibuni lilisababisha vifo vya watu 300 na wengine kujeruhiwa huku 56 hawajulikani waliko.

Chanzo cha usalama ambacho hakikuata jina lake litajwe kimesema ziara ya Bw. Farmajo nchini Uganda inaweza kuwa ni moja wapo ya jitihada za Somalia kuomba usaidizi zaidi wa kijeshi kutoka Uganda.

Mashambulizi ya kundi la Al Shabab yameua maelfu ya watu na wengine wengi wamelazimika kuyahama makazi yao na kukimbili nchi jirani, hasa nchini Kenya.