CAR-UN-USALAMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati

Waislamu waliokimbilia katika kambi ilio karibu na Msikiti wa Bangassou, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Agosti 14, 2017.
Waislamu waliokimbilia katika kambi ilio karibu na Msikiti wa Bangassou, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Agosti 14, 2017. Alexis HUGUET / AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa Jumanne, Oktoba 24 mjini Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ziara rasmi ya siku 4.

Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres anazuru Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati ambapo nchi hii inakabiliwa kwa mwaka mmoja sasa na vurugu zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.

Ziara hii ya Bw. Guterres nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inakuja wakati ambapo muhula wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo utaongozwa mwezi ujao na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kama hali ya hewa itaruhusu, siku ya Jumatano, Oktoba 25 Antonio Guterres atazuru Bangassou, eneo kunakoshuhudiwa machafuko kati ya makundi yenye silaha.

Mnamo mwezi Mei, jiji hili lilishambuliwa na kundi la wanamgambo waliojihami kwa silaha ambao waliwashambulia Waislamu. Watu zaidi ya 120, ikiwa ni pamoja na Walinda amani 6, waliuawa, maelfu ya watu walikimbilia katika nchi jirani ya DRC. Waislamu waliobaki katika mji huo, ambao bado wanatishiwa na wanamgambo hawa, wanaishi chini ya ulinzi wa Kanisa Katoliki.

Kama vile Bangassou, miji mingine na vijiji vingi vililengwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha katika miezi ya hivi karibuni, bila hata hivyo kukatazwa na na kikosi cha Umoja wa Mataifa. Minusca imekua ikikosoa kwa sababu ya uwezo wake wa kulinda raia kama inavyagizwa na mamlaka yake. Wanasiasa wengi, viongozi wa kidini na wawakilishi wa vyama vya kiraia watakutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ziara yake hiyo.

Katika hali ngumu ya kifedha kwa shughuli za kulinda amani, katibu mkuu ataomba askari 900 wa ziada mwezi ujao, ili kuimarisha kikosi cha askari 10,000 ambao tayari walitumwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.