UFARANSA-MALI-HAKI

Mauaji ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon: Uchunguzi haujazaa chochote

Claude Verlon (kushoto) na Ghislaine Dupont, Kidal, Mali, Julai 2013.
Claude Verlon (kushoto) na Ghislaine Dupont, Kidal, Mali, Julai 2013. RFI

Ni miaka minne sasa tangu kuawa kwa waandishi wa habari wawili wa RFI Claude Verlon na Gislaine Dupon, kaskazini mwa Mali. Ndugu wa karibu wa familia hizo wanalaumu vyombo vya sheria kutopiga hatuwa kuchunguza mauaji ya wapendwa wao.

Matangazo ya kibiashara

Miaka minne tangu kutokea kwa mauaji hayo, kumekuwa na kutatanisha kuhusu kufahamu ukweli kuhusu mazingira ya mauaji hayo.

Pierif shneder, msemaji wa shirika la marafiki wa Gislaine Dupon na Claude Verlon amesema ni bora zaidi kuharakisha uchunguzi ili ukweli ujulikane.

Siku hii inakuja wakati hii leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili na uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari.

Takwimu inaonyesha kuwa katika karne hii ya 21 zaidi ya waandishi wa habari wameuawa wakati wakitekeleza jukumu lao la kuhabarisha umma kuhusu matukio mbalimbali.

Orodha ya majina ya wanaofahamika na wasiofahamika ni ndefu na watakumbukwa kama vile Anna Politkovskaïa aliuawa jijini Moscou mwaka 2006, Claude Verlon na Gislaine Dupon waliouawa mjini Kidal nchini Mali Miaka minne iliopita, Christophe Nkezabahizi alieuawa na familia yake nchini Burundi, Robert Chamwami Shalubuto alieuawa mjini Ituri, DRC.

Kitendo hicho cha kutoadhibu wahusika kinachangia kuendelea kwa matukio mbalimbali ambapo makundi ya waasi yamekuwa mstari wa mbele.

Siku hii ya kimataifa ya kupinga Ukatili na Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari, ilianza kuadhimishwa mwaka 2013 baada ya Umoja wa Mataifa kuguswa na matukio ya mauaji hususan mauaji ya Claude Verlon na Guslaine Dupon.

Kuhusu lengo la kuuawa kwa wenzetu, hakuna maelezo kutoka upande wa serikali ya Ufaransa na ile ya Mali. Lakini Jaji Herbaut, ambaye alichukua nafasi ya Jaji Trédicdic, aliamua kukataa wazo la kulipiza kisasi ambalo lilihusishwa kwa upande mmoja na malipo ya fidia kwa ajili ya kuachiwa huru kwa mateka wa Arlit. Dhana hii ilitolewa kwenye taarifa ya mwezi Januari mwaka huu kwenye kituo cha France 2.